Unaweza kuona malipo yako ya awali na yajayo ya Showmax katika Akaunti yako.
- Nenda kwenye Showmax.com na uingie kwenye akaunti.
- Nenda kwenye Akaunti kupitia upau wa menyu wa juu kulia.
- Chagua Mipango na Malipo.
- Telezesha chini hadi kwenye Malipo Yajayo. Hapa unaweza kuona malipo yoyote yaliyoratibiwa.
- Chagua Angalia Historia ya Malipo. Hapa unaweza kuona malipo yako ya awali.
Ukigundua matatizo yoyote ya malipo, usisite Kuwasiliana Nasi.